Kupitia Instagram leo msanii Tunda Man ameweka picha ya msichana na ambae anadhaniwa kua ni mpenzi wake. Picha hiyo ambayo Tunda Man aliirepost kutoka kwa mwanadada huyo ajulikanaye kama Ameigh Thompson ilikua na maneno haya " Mwanaume anaye kufanya ujihisi ni muhimu....anayekufanya uwe na furaha basi wewe mwanamke...❤ " ambayo moja kwa moja yalimhusu Tunda Man
Kwa uchunguzi mdogo uliofanywa na BongoClan ni kua mpenzi wake huyo anaishi nchini Afrika Kusini na taarifa kutoka kwa mmoja wa marafiki wa Tunda Man zinasema kua mara nyingi Tunda hua anaenda Afrika Kusini kumtembelea mpenzi wake huyo.
Unaweza kutazama picha za mpenzi wa Tunda Man hapa chini na uone jinsi alivyo mrembo.