Mrembo na mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo ameamua
kuwapa makavu laivu magazeti hayo kwa kile ambacho Lulu anadai wamekuwa
wakimbandika kwenye kurasa zao ya mbele kila leo kwa stori za
kuungaunga.
“Okay...Acha nitoe PROMO bila Malipo tu maana inawezekana watu wana uhitaji...
Kwahyo kuna Magazeti yanaitwa VISA Na LETE MAMBO (tutambue uwepo wao
kwanza) Sasa Sina uhakika kama ni masharti ya Boss zao Au ni sheria yao
kutopitisha muda bila sura yangu kwenye magazeti yao tena Kwa story za
kujitungia tu...Sitaki mnidhihirishie Kwamba bila SURA YANGU kwenye
makaratasi yenu biashara haifanyiki....mtajiuliza Kwann nimekuja
kuwaweka insta,mnajua sababu....mnajifanya ni ma bingwa wa kuchukua
Habari kwenye mitandao Ya kijamii Na kuziboresha kwa uongo...Ichukueni
na HII basi....!!
Kama kweli mna uhakika hata bila sura yangu kwenye makaratasi yenu
kazi/biashara itakuwepo kama kawaida naomba mnidhihirishie hata ndani Ya
miezi 3 tu....otherwise Basi niwe boss wenu mana bila mimi hamna
mishahara...!
Endeleeni na madudu yenu...ila msije kukaa kwenye RIGHT ANGLE Mta Love show..!
NAJUA MTAPITA TU Cjui kama mna account humu ningewatag kbsa..!”-Lulu aliandika kwenye ukursa wake wa Instagram.
Bila shaka ujumbe umefika, ila nadhani hii pia kwao itakuwa stori pia.
Mzee wa Ubuyu