Shilole amedai kuwa mpango wake ni kumzalia mchumba wake Nuh Mziwanda watoto wawili.
Muimbaji huyo mwenye watoto wawili wa kike amesema hayo wakati akiongea kwenye kipindi cha The Mboni Show.
“Nitamzalia watoto wawili, nina wawili,” alisema Shilole aliyeongeza na
mchumba wake huyo kwenye kipindi hicho kinachorushwa TBC1. Shilole
amesema kuwa kadri siku zivyonaenda anazidi kumpenda zaidi Nuh kutokana
na mapenzi anayomwonyesha.
Mwaka jana Nuh alimvisha pete mchumba wake huyo.