ICON wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na Zari.
ICON wa
Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati aliamua kumtolea uvivu,
aliyewahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’,
King lawrenc kwa kumuita mpuuzi anayetafuta kiki kwa vile kila kukicha
kazi yake ni kumfuatafuata kwa maneno ya kejeli na kumtusi.

X wa Zari, King lawrence akipozi.
Akipiga
stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, staa huyo alisema mara
nyingi amejitahidi kumpuuza kwa kitendo chake cha kumkejeli katika
mitandao ya kijamii, lakini kitu alichogundua ni kwamba mpenzi huyo wa
zamani wa Zari anataka yeye amjibu ili aweze kulikuza jina lake, kitu
ambacho ni cha kijinga.

Zarinah Hassani ‘Zari’.
“Nimejitahidi sana kukaa kimya kila
anaponitusi huyu jamaa, lakini kumbuka mimi ni binadamu, najaribu
kuliangalia jambo hili nagundua kwamba hana chochote cha msingi
anachoongea zaidi ya matusi, anatafuta nimjibu kitu ili apate kiki
aweze kutimiza ndoto zake,” alisema Diamond na kuongeza:
“Nashukuru nimegundua hana mada ya kuzungumza
katika mitandao zaidi ya mimi na Zari, ningemshauri aendelee na
shughuli zake za kila siku, asihangaike na kitu asichokijua, kugombana
na mimi ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, mimi nawaza nifanyeje ili
niweze kuitangaza nchi yangu, yeye anawaza afanyeje ili aweze kupandisha
jina lake, siwezi kubishana na mpuuzi.”
Mwanaume huyo Mganda, kwa muda mwingi amekuwa
akiweka picha zake, Zari na Diamond akisindikiza na maneno ya kejeli na
dhihaka dhidi ya mkali huyo wa Bongo Fleva, katika kile kinachoonekana
kuwa ni kushikwa na wivu.