TAARIFA KWA UMMA
BENKI YA I&M YAZINDUA HUDUMA YA KWANZA YA MFUMO
WA KIELEKTRONIKI YA MASAA 24 KATIKA JENGO LA VIVA TOWERS, POSTA JIJINI
DAR ES SALAAM
Jumanne 03/02/2015: I&M Bank (T) Limited imeendelea kuonyesha muelekeo mzuri katika
soko baada ya kuzindua huduma ya kwanza na ya kipekee ya ya kibenki
ijulikanayo kama “Banking lounge” itakayokuwa ikifanya kazi
kwa masaa 24 kwa siku saba, ndani ya ghorofa ya kwanza katika jengo
la Viva Towers, moja kati ya maeneo muhimu jijini Dar es salaam. Tanzania.
Hili ni jaribio
la kipekee kwa Benki hiyo, kutoa huduma mbalimbali za kibenki kama vile;-Mashine
ya kubadilisha fedha za kigeni, mashine ya mfumo wa ATM ya kuweka na
kutoa fedha, “Siku yoyote, muda wowote” ndani ya masaa 24 katika
siku saba za wiki.
MASHINE YA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI: Ni sehemu ya kubadilishia fedha itakayokuwa ikifanya kazi kwa muda
wa masaa 24 ndani ya siku saba za wiki. Hii itamuwezesha mteja kubadilisha
fedha zake za kigeni na kupokea shilingi ya kitanzania bila ya kuwa
na mtoa huduma. Hii itakuwa na umuhimu zaidi kwa wateja ambao watapenda
kufanya miamala yao hasa nyakati za jioni/usiku huku kukiwa hakuna haja
ya mteja kuwa na akaunti ya benki hiyo pindi anapotaka kupata huduma
hii bali anachohitaji ni pasipoti halali ili kupata huduma.
MASHINE YA KUWEKEA FEDHA: Itamsaidia mteja kupata huduma kwa masaa 24 ndani ya siku saba hasa
kwa maduka na biashara yanayofungwa mida ya jioni/usikuili kuweka fedha
za mauzo yao ya siku nzima katika akaunti za benki zao muda wowote.
Huduma hii ni ya kila siku ikiwemo siku ya jumapili na siku za sikukuu.
Benki hii imefunga “kifaa maalum cha kuwekea fedha”, ambacho kiasi
chochote kikubwa cha fedha kinaweza wekwa kwa usalama wa hali ya juu
katika mashine hiyo pasipo na uhitaji wa mtoa huduma wa benki.
Mashine hii itahesabu
fedha na itatoa risiti kwa mteja. Mashine hii ina kasi ya ajabu na uwezo
mkubwa wa kuweka fedha nyingi, ikiwa na teknolojia ya hali ya juu kama
vile kitambua fedha endapo itakua ni feki au la, kichambuzi na kitambuzi
namba n.k.
MASHINE ZA ATM: Mashine za ATM zilizowezeshwa na VISA zitakazokuwa zikifanya kazi
kwa masaa 24 zitawahudumia wateja na wa watumiaji wa kadi za VISA.
Zaidi ya huduma
hizi za hali ya juu, Benki pia imeanzaisha “VIP SERVICE LOUNGE” ambayo inatoa huduma
ya kibenki isiyo ya fedha, katika hali ya kisasa na starehe. Ikiwa na
TV na mashine za kujipatia kahawa, mteja anaweza kukaa na kupumzika,
katika hali salama, wakati wahudumu waliofunzwa kwa umahiri wakiendelea
kumhudumia, kuanzaia saa 2 asubuhi mpaka saa 2 usiku. Pia wahudumu watasikiliza
na kupokea mahitaji yote ya wateja yatakayotolewa huduma katika tawi
letu la Maktaba kama vile:-maombi ya kufunguliwa akaunti, maombi ya
TT/TISS, huduma za vitabu vya hundi, kadi za malipo ya kabla ya fedha
za kigeni, huduma ya kadi za ATM, mikopo, maombi ya kadi za BPesa, taarifa
nyingine za kibenki na msaada katika huduma nyingine za kibenki.
I&M imekuwa
ni benki ya kwanza kuanzisha huduma hii ya teknolojia ya hali ya juu
katika soko la Tanzania ambapo “Smart Banking Solutions Ltd” kwa
mara nyingine tena imepiga hatua kwa kuungana na benki hiyo na kufunga
mashine za kuweka na kutoa fedha sambamba na kubadilishia fedha za kigeni.”
.
Akielezea faida
za mfumo huu, Afisa mtendaji mkuu wa benki ya I&M Bw. Anurag
Dureha alisema “Kwa mfumo huu mpya mteja wa I&M sasa atakuwa
na uwezo wa kutumia huduma za kibenki kwa urahisi”. Tawi hili jipya
linampa mteja njia mbadala za kufanya miamala, zaidi ya ile ya awali
kama vile matawi ya benki, intaneti na simu za mikononi.
“Kwa kuanza,
fedha ya kigeni itakayobadilishwa na mashine hizi ni dola za kimarekani
muda mfupi baadae tutaongeza fedha nyingine za kigeni ili kutimiza mahitaji
ya wateja wetu wanaotoka sehemu mbalimbali duniani kote” aliongeza
Bw. Dureha.
aaaa