MWAKA mpya tayari imeanza huku kila mtu amemaliza tathamini kwa mwaka uliopita 2014, na sasa ni 2015 mwaka wenye matarajio mengi huku kisiasa ukionekana kuwa ni mwaka uliojaa matukio mengi ambayo ni makubwa kura katiba pendekezi pia uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge.
Tunaingia mwaka huu tukiangazia wasanii ambao wanatarajia kufanya vinzuri katika tasnia ya filamu na kuibuka vinara katika tasnia huku pia wengine wakilinda nafasi zao ambazo wamejitengenezea kwa muda mrefu au mwaka uliopita.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni msanii anayetarajiwa kuteka soko la filamu baada ya kuwa na mkataba na kampuni ya Proin Promotion inayomuandalia filamu kubwa kimataifa ratiba inaonyesha kuwa mwaka huu ndio atarekodi na kuingia sokoni ndani na nje ya Tanzania.
Akiongea hivi karibuni Lulu alisema kuwa nia yake ni kutafuta tunzo nje ya nchi baada ya ndani kutokuwa na tuzo kubwa kwa kila mwaka anatarajia kutengeneza filamu itakayompeleka katika tunzo za Oscar.
Msanii mwingine atakayefanya vinzuri kwa mwaka huu ni Salma Jabu ‘Nisha’ mwanadada ambaye amekuwa nyota kwa mwaka uliopita katika uandaaji wa filamu zinazotikisa soko la filamu Swahilihood kwani kila siku amezidi kufanya vinzuri na anatarajiwa kufanya vema kwa mwaka 2015.
Salim Ahmed ‘Gabo’ msanii mwenye msimamo kwa sasa anazidi kuwa bora kwani Gabo hashiriki filamu bila kusoma muswada (Script) na kukubali kama ni sinema ambayo itamfanya awe bora kwa kushiriki katika filamu husika naye tunaamini kuwa atafanya vema mwaka huu.
Pamoja na kutangaza mara kadhaa kutaka kustaafu kuigiza filamu Amri Athuman ‘King Majuto’ amezidi kuwa nguzo kwa wasanii wote kwani sinema anazoshiriki zote zimekuwa zikifanya vinzuri katika mauzo sokoni, pamoja na kushiriki kazi nyingi bado hajashuka katika uigizaji.
King Majuto anafanya vinzuri na mwaka huu ataendelea kufanya vinzuri hadi hapo atakapoamua kustaafu rasmi kama ambavyo amekuwa akisema alipoongea na Mwanaspoti alisema kuwa moja ya sababu ya kutangaza kujiudhulu ni maslahi ya filamu kutosimamiwa na Serikali vinzuri.
Shamsa Ford toka kutoka kwa filamu yake ya Chausiku nyota yake imezidi kung’ara na kuzidi kufanya vinzuri sokoni anatarajia kuingia na kazi ambayo itamfanya ateke soko kwa mwaka 2015 na kuwa ni moja kati ya wasanii watakaofanya vinzuri.
Omary Clayton msanii aliyeibuka na filamu za majonzi anatarajiwa kufanya vinzuri kwa mwaka huu kwani amekuwa mahiri sana katika sinema zinazohuzunisha kwa wapenzi wa filamu wanaopenda filamu za kijamii mwaka 2015.
Riyama Ali ni msanii ambaye kwa muda mrefu amedumu kuwa mahiri katika uigizaji kwa kubadilika badilika katika uhusika ana uwezo wa kucheza nafasi yoyote katika filamu kitu kinachomfanya asishuke katika nafasi ambayo amekuwa nayo kwa muda mrefu katika tasnia ya filamu atafanya vinzuri kwa mwaka 2015.
Wastara Juma mtayarishaji wa filamu ameendelea kusimamia kampuni aliyoachiwa na marehemu mumewe Sajuki Wajey Film amemaliza mwaka huu kwa kufanya filamu kama Uaminifu dhaifu inayofanya vema katika tasnia ya filamu Swahilihood kwa mwaka huu 2015 anaingia na nguvu mpya.
Changamoto iliyopo kwa wasanii wengi ni mfumo wa ununuzi wa filamu kwa wasambazaji ambao wamekuwa mara nyingi wakihitaji sura zile zile zikijirudia lakini kwa sasa mambo yamebadilika wasanii wanaobahatika kuingia filamu mpya na kuwafunika wasanii wakongwe.
Pia mwaka 2015 umeingia vibaya baada ya mvutano uliopo kati ya wasambazaji wachanga na kampuni kubwa inayoshikilia wasanii wengi na watayarishaji wakubwa katika tasnia ya filamu Tanzania

KWAHISANI YA FC