WATU wawili wamefariki dunia jijini Dar es Salaam juzi akiwamo Emmanuel Ndahani (39) mkazi wa Kibamba, aliyegongwa na gari na kufariki dunia alipokuwa akiweka alama za matawi kuzuia gari zisikanyage maiti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema Ndahani aligongwa na gari isiyofahamika kwa kuwa lilikimbia baada ya ajali hiyo.
Alisema Ndahani alikuwa akitaka kuzuia magari yasiukanyage mwili wa Onesmo Yarimunda aliyefariki dunia baada ya kugongwa na basi la Prince Muro alipokuwa akivuka barabara.

Kamanda Wambura, alisema Yarimunda (36), mkazi wa Kibaha aligongwa na basi hilo aina ya Scania, juzi, saa 3 usiku maeneo ya Kibamba.
Maiti zimehifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha. Dereva wa basi la Muro, Boniface Chuwa (36) mkazi wa Kibaha anashikiliwa na polisi.
 
Top