Mwanamuziki ambae ni dada na Diamond Platnum Queen Darleen amezidi
kuchochea chuki na bifu kwa mashabiki wa Ali Kiba na Diamond Platnum
baada ya kupost maneno ambayo mashabiki hao wanaona ni kama anazidi
kuchochea bifu iliyopo kwa mashabiki wa wanamuziki hao ambao kwa sasa
wamekuwa na ushindani mkubwa kimuziki.
Mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwa na show kubwa ya muziki ambayo
ilifanyika katika viwanja vya Ledears Club ambapo katika show hiyo
iliwakutanisha Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba ambao kila mmoja
alipata mapokezi tofauti kutoka kwa mashabiki wao.
Katika show hiyo kuna baadhi ya mashabiki ambao walikuwa na furaha
kushuhudia show ya wakali hao wawili wakati show inaendelea msanii
Diamond Platnum aliweza kuwarushia noti za buku mbilimbli mashabiki
wake.Kufuatia kitendo hicho ndipo msanaii Queen Darleen amefunguka na
kusema kuwa dawa ya machupa stejini ni pesa. "Machupa kiboko yake pesaa,tunasaka hela na wewe saka "
Mashabiki wa Queen Darleen wameonyeshwa kutofurahishwa na kauli ambayo
imetolewa na dada wa nyota wa muziki Diamond Platnum na wao wanaamini
kuwa msanii huyo anazidi kuchochea bifu iliyopo kwa mashabiki wa Diamond
pamoja na Ali Kiba