Tukirudi nyuma na kuangalia visa kadhaa vya Wanamuziki maarufu duniani
ambavyo vilipelekea kupoteza maisha ya watu. Mfano mzuri ni wa Tupac
Amaru Shakur na Christopher George Latore Wallace akijulikana kama The
Notorious B.I.G., Biggie or Biggie Smalls.
Beef la 2Pac na BIG ilivyoanza
Walikuwa marafiki, walifanya show pamoja, walifanya interviews na kutoka pamoja, walibadilishana uwelewa wao / mawazo kuhusu game hiyo ya Hip Hop huku wakifundishana baadhi ya vitu.
Lakini vyote hivi vilitenganishwa baada ya kutokea shambulio la risasi mjini New York ambako 2Pac alikuwa ana rekodi. Inavyosemekana kuwa muda ambao risasi ilirushwa Biggie pamoja na P.Diddy walikuwepo . 2Pac alimtuhumu Biggie kuwa ndie alietengeneza mpango huo na hapo ndipo mahusiano yao yalipoanza kupungua.
2Pac alimtuhumu Big kuwa alimset na alikuwa na sababu ya kufanya hivyo, maana hao wawili ndio walikuwa Rapper wakubwa na wakali nchini USA, huku akiamini kuwa sababu kubwa ya tukio hilo ni mbinu za Big kumshusha katika ramani ya Game.
Lakini tunaona baadae vita iliendelea na kusambaza chuki mpaka kwenye makundi yao East Coast na West Coast, na hapo ndio beef ilizidi kuwa kubwa na kupelekea mauaji ya Rapper hao.
Diamond na Alikiba
Hawa nao wameanza kushirikiana pamoja na kufanya shughuli zao kwenye studio moja kwa muda mrefu tu, sitaki kugusia deep sana chanzo chao lakini baada ya Diamond kuondoka kwenye uongozi wake wa Studio alipokuwa mwanzo ndipo hali ilianza kubadilika kimya kimya.
Alikiba alifanya vizuri kwenye muziki huku Diamond nae akija kwa kasi, so kukawa na challenge hapo kati lakini mwisho wa siku kila mmoja alifanya vizuri kwa uwezo wake na kila mmoja alitamani kuwa wa kwanza / bora zaidi ya mwenzie.
Yakapita matukio mengi lakini mpaka kufikia leo kuwa na matabaka mawili makubwa kama ilivyokuwa East na West Coast enzi za Big na 2Pac, ambapo sasa kuna team Kiba na Team Diamond kwenye mitandao ya kijamii hata mitaani pia ushabiki huo umeendelea kukua kwa kasi na kujenga chuki kwa msanii wa upande wa pili.
Chuki hii imezidi kujidhihirisha kwenye matamasha mawili yaliyotokea hivi karibuni ambapo mashabiki wa Msanii A wanachukua maamuzi ya kumrushia chupa za mikojo, mawe n.k msanii B, na kupelekea mashabiki wa Msanii B nao kulipiza kwa Msanii A. Inasemekana kuwa wasanii wenyewe ndio wanawalipa ama kufanya mipango hivyo ili kumpoteza mwengine.
www.hassbabytz.com
Pengine ni Beef ya maslahi kutengeneza pesa au kuendeleza majina lakini ukweli wanaujua wao wenyewe. Ila mwisho wa siku chuki inazidi kuenezwa na inapoelekea ni hatua mbaya. So ni vema kwa watu ambao wana hekima na wadau wakubwa wa Muziki huu wa Bongo Fleva kuwaweka chini pamoja wasanii hawa na kumaliza tofauti zao na tena ikiwezekana kutengeneza wimbo wa pamoja kama kurudisha amani kwao na kwa mashabiki wao.
Pia kuna baadhi ya watu ambao kwa imani yangu naona wanachochea au kukuza beef hii, mmoja wapo ni huyu anaesemekana kuwa ni Meneja wa Diamond sijafahamu jina lake halisi but anatumia (SK), baada ya kufatilia post zake kadhaa nimeona ni vema ku share nanyi wadau wangu. Hizi hapa chini
Sidhani kama Manager wa msanii mkubwa kama Diamond ametumia busara au alipaswa kuandika hivyo badala yake angetumia hekima kutatua jambo hilo lakini si kwa njia ya kuandika kwenye social network ambapo inazidi kuchanganya mashabiki na kuongeza mashabiki wapya ambao wataelekeza chuki kwa mwengine. Ni vema jamaa akajitambua yeye ni nani na anapaswa kutatua jambo kwa njia ipi sahihi, Au ajifunze hata kwa Saidi Fella Manager ambae sijawahi sikia akiropoka au kuongea jambo ambalo litazaa chuki baadae badala yake hutumia kauli tulivu.
Pia media, kampuni na mashabiki waache kuchochea hizi beef nadhani hapo amani itapatikana na kila msanii atafanya show yake kwa furaha bila hofu ya kurushiwa chupa.
Diamond anaweza na Alikiba pia anaweza na wote ni wasanii wa Tanzania hivyo ni vema tukawa support wote.
*Kumradhi kwa wote ambao nimetumia majina yenu humu.
Credit : HassBaby Blog