 |
Meninah |
habari mpya zinasema kuwa vikao vya harusi ya Diamond na Meninah ambaye
ni mwanamuziki wa Bongo fleva vimeanza kimya kimya nyumbani kwa mama
Diamond huku mmoja wa wahudhuriaji wakiwa ni mama Diamond mwenyewe na
Queen Darling ambaye ni dada wa Diamond.
Kwa mujibu wa
Baabkubwa magazine
paparazzi wake alienda nyumbani kwa Diamond hivi juzi kati kufanya nae
mahojiano hata hivyo hakumkuta Diamond lakini alimkuta mmoja wa watu
wake wa karibu ambaye yupo pia upande wa Wema Sepetu.
Chanzo hicho kilimwaga news kuwa hakuna cha ndoa ya Diamond na Wema bali
ndoa inayopangwa kwasasa ni ya Diamond na Meninah na vikao vimeanza kwa
mama Diamond. Chanzo hicho kilisema kuwa Diamond na Meninah walikutana
takribani miezi mitano iliyopita wakati wa maandalizi ya tuzo za Kili
Awards 2014 ambapo wote walitumbuiza. Baada ya hapo wakaingia mapenzini
kimya kimya mpaka wiki za hivi karibuni gazeti moja lilipovujisha habari
hizo za mahaba ya Diamond na Meninah na media nyinmgine kuziandika kwa
kasi.
 |
Meninah |
Kwa mujibu wa chanzo hicho ni kuwa Wema ametoswa sababu ya kuendekeza
pombe inayompelekea kuwa mvivu na kutotaka kufanya kazi badala yake ni
starehe tupu, kwa maana kuwa hata nyumbani kwa mama Diamond haendi mara
kwa mara kumsalimia inaweza hata kupita miezi 3 hajaenda ila Meninah
anaenda na akifika kule humsaidia mama Diamond kazi, kupika na kupakua.
Chanzo hicho kimesema kuwa hata Wema anajua kuwa Diamond na Meninah wana
ishara zote za kuwa wapenzi lakini hana cha kufanya, huku Meninah yeye
akiwa tayari amejitoa muhanga kwa Diamond lakini anawaogopa Team Wema
kumshambulia hasa kwa mvua za matusi kama ilivyo kawaida yao lakini mama
Diamond anampoza kuwa asiwe na shaka yeye kamkubali Diamond hawezi
kukataa kumuoa hilo amuachie yeye mama Diamond.
Vikao hivyo licha ya kuhudhuriwa na mama Diamond na Queen Darleen,
chanzo hicho kimesema pia kuwa kuna ndugu wengine wa Diamond na mama
Diamond wanahudhuria ila yeye hawajui sababu hana ukaribu nao.
Wema na Diamond