SERENGETI BREWERIES LTD
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Shinyanga, Tanzania-Septemba 12/2014
BAADA ya kufanya
maonyesho ya kuvutia katika zaidi ya mikoa sita nchini, shughuli hiyo ya
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) bado kabisa haijamalizika, na sasa macho yote
yameelekezwa kwa wakazi wa Shinyanga ambao wanasubiri kwa hamu kubwa kufahamu nini watapata kutoka Serengeti fiesta
leo.
Upo uchangamfu wa aina
yake kwa mashabiki wa hapa; kwa hakika karibu wakazi wote tuliokutana nao
wamekwishajiandaa kuhudhuria shoo hiyo mbali na ukweli kuwa Serengeti Fiesta
imekuja mkoani humu kwa kuchelewa kuliko ilivyotarajiwa. Onyesho la Serengeti
Fiesta mjini Shinyanga lilipaswa kufanyika Septemba 6 mwaka huu kwenye Uwanja
wa Kambarage, lakini likaahirishwa kutokana na ajali mbaya iliyotokea mkoani
Mara ikihusisha magari matatu.
Wakazi wengi wa
Shinyanga wamefurahia na kuipongeza timu nzima ya SBL kwa kujitolea
kushirikiana na jamii wakati wa ajali hiyo iliyoua karibu watu 40, na kuzitaka
kampuni nyingine kuiga mfano huo.
Timu ya SBL pamoja na
wasanii waliwatembelea majeruhi hospitalini na kuzifariji familia zilizopoteza
wapendwa wao, ambapo walichangia chakula na vitu vingine muhimu.
Katika kuonyesha kuwa
SBL ipo nyuma ya kaulimbiu ya mwaka huu ya Serengeti Fiesta isemayo;
‘SambazaUpendo’, mapato ya mlangoni kwenye onyesho la Serengeti Fiesta 2014
mjini Musoma, yalipelekwa kwa familia zilizoathirika na janga lile la ajali.
Young Killa, Fid Q na Stamina wakiongozana na zaidi ya wasanii
wengine 10 wenye vipaji vya hali ya juu, wameahidi kufanya onyesho la nguvu
kwenye Uwanja wa Kambarage. Orodha ya wanamuziki hawa inawajumuisha pia akina
Ommy Dimpoz, Linah, Recho, Ney wa Mitego, Chege na Temba, Nikki II, Mo Music na
Kadja, ambao watasindikizwa na wasanii wenyeji wa mkoa wa Shinyanga.
Wakati maandalizi yakipamba moto, tulikutana na Meneja wa Kinywaji
cha Serengeti, Bw. Rugambo Rodney, aliyekuwa na machache ya kuwaambia wakazi wa
Shinyanga: “tiketi zipo tayari na maandalizi yanaendelea, ningependa kuwatia
moyo wanaShinyanga, wahudhurie kwa wingi kwani tuna akiba ya vitu vingi na
mambo makubwa kwa ajili yao.”
Baada ya Shinyanga, Serengeti Fiesta 2014
itakuwa njiani kuelekea Geita ikiwa ni mwendelezo wa maonyesho 18 yaliyoahidiwa
kwa mashabiki.
About
Serengeti Breweries Limited
Serengeti Breweries
Limited engages in the brewing, manufacturing, marketing and selling drinks
made of malt, hops and barley and sorghum in Tanzania.
Headquartered in
Dar es Salaam, SBL brands include:- Serengeti Premium Lager, Serengeti
Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner
Lager, Senator, The Kick and Guinness®.
SBL is also the
sole distributor of several international renowned spirits including Smirnoff
Vodka®, Johnnie Walker®, Bailey’s Irish Cream ®, Richot®, Bond 7 Whiskey® and
Gilbeys Gin®.
Serengeti
Breweries Limited is a subsidiary of East African Breweries Limited/ DIAGEO
PLC.