BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???




Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri, Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava Nasib Abdul 'Diamond Platnumz' alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.
Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake Mr.Awin Williams Akipomiemie raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
 
Hapo ndipo washabiki hao walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake.
 
Kilichowakera zaidi mashabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo hosptalini kwa sasa.
 
Moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake, mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatal.
 
Polisi nchini Ujerumani wamesema tukio hilo la aibu halijawahi kutokea, kwani msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari sana kwani mashabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
 
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Kupitia Instagram Diamond alidai kusikitishwa na tukio hilo.
 
Kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany… kinachoniuma na kunisikitisha zaidi ni jins watu walivyoamua kujitolea kuja kwa wingi kutusupport vijana wao, halaf mwisho wa siku promoter anatupeleka wasanii kwenye show saa kumi alfajiri… najua ni kiasi gani mmeumia na kuwa disappointed… lakini naomba mtambue kuwa halikuwa ni kosa langu, coz mimi ni mgeni tu, na nafata maelekezo ya promoter…hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaoutaka mimi….