BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???


Siku kama ya leo miaka 35 iliyopita, Jean-Bedel Bokassa dikteta wa Jamhuri ya Afrika ya Kati aling'olewa madarakani katika mapinduzi yaliyotokea nchini humo. Alizaliwa mwaka 1922 na kusomea nchini Ufaransa. Bokassa alikuwa shabiki mkubwa wa Napoleon Bonaparte na Charles de Gaulle, viongozi wawili wa zamani wa Ufaransa. Bokassa alichukua madaraka mwaka 1966 baada ya kumpindua binamu yake David Dacko, wakati huo Bokassa akiwa mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Jean-Bedel Bokassa aliiongoza Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa utawala wa kiimla kwa kipindi cha miaka 13 huku akiongoza na kusimamia moja kwa moja wizara 14 kati ya wizara zote 16 za nchi hiyo. ***
Miaka 183 iliyopita katika siku kama ya leo, basi la kwanza lililokuwa likitumia nishati ya mvuke liliundwa. Basi hilo jipya ambalo lilikuwa likitembea kwa kutumia nishati ya mvuke lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 30 huku likienda kwa mwendo mdogo. Basi hilo liliundwa na raia wa Uingereza. Miaka kadhaa baadaye kulitengenezwa mabasi bora na ya kisasa zaidi yanayotumia nishati ya petrol. Hii leo mabasi ni miongoni vya vyombo muhimu vya usafiri wa umma. ***
Katika siku kama ya leo miaka 147 iliyopita Hungary iliungana na ardhi ya Austria na Francois Joseph akawa mtawala wa kifalme wa nchi mbili hizo. Hungary ambayo kwa mara kadhaa katika historia ilivamiwa na kukaliwa kwa mabavu na madola yenye nguvu ya Ulaya kama Austria na utawala wa Othmania, hatimaye ilipata uhuru mwaka 1918 mwishoni mwa Vita vya Kwanza vya Dunia. ***
Na siku kama ya leo miaka 1235 iliyopita kwa mujibu wa kalenda ya Hijria, Imam Ridha (a.s) aliondoka mjini Madina na kuanza safari yake ya kuelekea Marw kaskazini mashariki mwa Iran ya kale. Imam Ridha alifanya safari hiyo kwa lazima na mashinikizo ya Maamun Khalifa wa Saba wa utawala wa Bani Abbas. Lengo la Maamun kutaka Imam Ridha apelekwe Marw lilikuwa ni kumfanya awe karibu na hivyo kudhibiti nyendo zake. Japokuwa kidhahiri Maamun alimfanya Imam kuwa mrithi wa kiti, cheo ambacho Imam Ridha alikikubali kwa kulazimishwa, lakini uhakika wa mambo ni kuwa alitaka kuimarisha misingi ya utawala wake. Imam Ridha aliendelea kuutambua utawala wa Maamun kwamba, si halali na alikuwa akifichua uovu na dhulma za utawala huo. Hatimaye Maamun alishindwa kuvumilia shakhsia ya kielimu na kimaanawi ya Imam pamoja na ushawishi wake kwa watu, hivyo akaamua kumpa sumu na kumuua shahidi. ***