Mambo hadharani! Baada ya kimya kirefu, staa wa Hip hop
Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa mara ya kwanza amemwanika
mtoto aliyezaa na msanii wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ na
kukiri kwamba ni wa kwake.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Nay alisema kuwa anampenda
mwanaye huyo na kwa sasa anaishi naye nyumbani kwake. Kimara-Baruti, Dar
na ana umri wa miaka miwili na nusu anayejulikana kwa jina la Munie.

“Nampenda sana mwanangu ndiyo maana nimeamua kumchukua kwa
mama yake Skaina na kuja kumlea kwangu, analelewa vizuri sana na mama
yake ambaye ni Siwema namshukuru Mungu mwanangu anaendelea kukua,
nafurahia sana kukaa na mwanangu karibu tofauti na alivyokuwa kwa mama
yake,” alisema Nay wa Mitego.

Skaina aliwahi kukiri kuwa mwananye huyo baba yake ni Nay
lakini baada ya Nay kuulizwa alichengachenga hivyo sasa ameamua kumuweka
wazi.