BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???


Siku kama ya leo miaka 54 iliyopita, hati ya Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC) ilitiwa saini na nchi za Iran, Saudia, Iraq, Kuwait na Venezuela. Jumuiya hiyo ilianzishwa kwa lengo la kukabiliana na makampuni makubwa ya mafuta ya Magharibi ambayo yalikuwa yakisimamia uvumbuzi, uchimbaji na uuzaji wa bidhaa hiyo kimataifa na kuainisha bei ya bidhaa hiyo muhimu kwa maslahi yao binafsi na kwa madhara ya nchi zalishaji. Licha ya kwamba awali jumuiya hiyo haikuwa na nguvu wala ushawishi wowote, lakini ilikuja kupata nguvu zaidi baada ya nchi kadhaa zikiwemo, Algeria, Libya, Nigeria, Qatar, Imarat, Gabon, Indonesia na Ecuador ambazo ni wazalisha wa mafuta kujiunga nayo.

Siku kama ya leo miaka 202 iliyopita, moja kati ya ajali kubwa za moto ulimwenguni na uliowashwa makusudi ilitokea katika mji mkuu wa Russia Moscow. Tukio hilo lilitokea baada ya kupita siku moja tu, tangu mji huo uvamiwe na kukaliwa kwa mabavu na majeshi ya Napoleone Bonaparte, wakati mji huo ulipochomwa moto kwa amri ya mtawala wa wakati huo wa mji huo. Lengo la mtawala huyo lilikuwa ni kuyafanya majeshi ya Bonaparte yashindwe kustafidi na suhula za mji huo. Moto huo mkubwa uliteketeza na kuharibu kabisa robo tatu ya mji mzima wa Moscow.

Na siku kama ya leo miaka 62 iliyopita, alifariki dunia msomi mashuhuri wa Kiislamu na mtaalamu mkubwa wa fasihi, Ayatullah Hussein Kashiful Ghitaa. Ayatullah Kashiful Ghitaa alisoma masomo ya juu ya fiqhi na usuul fiqhi kwa wasomi wakubwa wa zama zake huku akitabahari pia katika elimu ya sayansi, falsafa na hadithi. Mbali na kuwa mtaalamu katika elimu za dini Ayatullah Hussein Kashiful Ghitaa alikuwa hodari katika mashairi huku akiacha tenzi kadhaa za mashairi katika uwanja huo. Akiwa kijana msomi huyo mkubwa wa Kiislamu aliingia katika masuala ya kisiasa na kuwa na taathira katika mapambano dhidi ya mkoloni Mwingereza.