Wanasema tumia pesa ikuzoee na hiki ndo alichokifanya mchezaji mpya wa Liverpool Mario Baloteli wakati akiwasili katika uwanja unaotumiwa kwa mazoezi na Timu ya Liverpool. Baloteli aliingia uwanjani hapo akiwa na gari aina Ferrari F12 Berlinetta ambayo inauzwa Pound 240,000 ambazo ni sawa na milioni 652 zakibongo.

Baloteli pia anamiliki gari nyingine aina ya Bentley GT ambayo inauzwa zaidi ya milioni 450 za kibongo. Baloteli ameamia Liverpool akitokea timu ya Ac Milan ambako alikua akichezea.

 
Top