Super Star kunako tasnia ya sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe (26), anadaiwa kuangua kilio kisa kutopata mtoto.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni
mtu wake wa karibu, staa huyo amekuwa akihaha kusaka mtoto huku
shinikizo likitoka kwa bibi yake, mzaa baba ambaye amekuwa akimuuliza
juu ya yeye kumpata mtoto kwani umri unazidi kuyoyoma.
Habari zilidai kwamba
mwanadashosti huyo alishakwenda kwa madaktari mbalimbali ambao walimtaka
kutokuwa na pupa kuhusiana na suala hilo na zaidi azidi kumuomba Mungu.
“Unajua umri ukishasogea,
wanawake wengi huwa na wasiwasi juu ya suala hilo la kupata mtoto kama
ilivyo ishu ya kusaka ndoa maana ni kati ya vitu vinavyowatesa.
“Wolper ana wataalam wake lakini hawajamwambia kama ana tatizo la kutopata mtoto.
“Kuna maelekezo ambayo wamekuwa wakimpa ambayo humrejeshea furaha anapowaza ishu hiyo.”
“Madaktari walimwambia tatizo la
kutopata ujauzito ina maana mwanaume na mwanamke au watu walio katika
uhusiano wa kutafuta ujauzito ndani ya mwaka mmoja wameshajitahidi
kufanya hivyo lakini wameshindwa.
“Walimwambia pia inaweza ikawa zaidi ya mwaka mmoja lakini wastani
kiwango cha chini ni mwaka mmoja ambacho Wolper alishakuwa na mwanaume
lakini hakufanikiwa ndiyo maana wakati mwingine anakuwa na hofu.
“Kuna wengine wanamwogopesha wanapomwambia kukosa mtoto ni tatizo
kubwa katika jamii kwani kila mwanamke anataka afikie malengo ya kuwa
na familia na hasa kunapokuwa na shinikizo la wazazi wanataka mjukuu.
“Katika maelezo yao,
madaktari walimwambia si mwanamke pekee anayeweza kuwa na tatizo bali
hata mwanaume, hivyo tatizo linaweza kuwa kwa hao wanaume aliowahi
kuchepuka nao,” chanzo kilimaliza kutiririka huku kikiomba hifadhi ya
jina.
Baada ya kujazwa data hizo, Risasi Jumamosi lilimsaka Wolper ambapo alipopatikana, alifunguka kila kitu juu ya ishu hiyo.
Akizungumza mara tu baada ya kutua Dar kwa ndege akitokea mkoani
Kilimanjaro ambako alikwenda kumsalimia bibi yake huko Old Moshi, staa
huyo alisema kwamba hakuna siku ambayo aliumia kama alivyokwenda
kijijini na kukutana na bibi yake na kuanza kumuuliza kuhusu lini
atapata mtoto.
“Kiukweli hakuna kitu ambacho kiliniingia kwenye moyo kama bibi yangu
kuniuliza kuhusu mtoto, nimejikuta nikitoa machozi tu. Ni kama
alitonesha kidonda,” alisema mdada huyo.
Wolper alisema kuwa bibi yake alimsisitiza kwamba asijali kuhusu
mtoto atakula nini bali akimpata ampeleke kwake kwani atakula chochote
atakachokula bibi huyo.
Katika maelezo mengine, Wolper alisema amejitahidi sana kutafuta
mtoto lakini imeshindikana lakini anamuamini Mungu kuwa atampata
kulingana na matakwa yake.
“Nimejitahidi sana kusaka mtoto lakini imeshindikana hivyo kwa wale
ambao wanabahatika kupata mimba nawashauri wasitoe maana mtoto ni faraja
kubwa kwa wanawake,” alisema Wolper.
Wolper aliongeza
kwamba aliyachukua maneno ya bibi yake kwa mikono miwili na atayafanyia
kazi, inawezakana mpaka mwakani anaweza kulikamilisha hilo lakini kuna
changamoto moja tu anayokumbana nayo nayi ni nani wa kuzaa naye ambaye
atakuwa baba bora wa mwanaye.
“Unajua
unaweza kuzaa mtoto wala isiwe tabu kumlea kabisa kwani wapo watu wengi
wanaweza kumwangalia, tatizo ni nani wa kuzaa naye tu jamani,” alisema
Wolper huku akiamini kuwa siku ikifika Mungu atamjalia mtoto.
Wolper aliwahi
kuripotiwa kutoka kimapenzi na wanaume kadhaa wakiwemo mastaa wa Bongo
Fleva, Ali Saleh Kiba, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Khalid Juma
‘Jux’ na yule mwanaume aliyezua naye tafrani kabla ya kumwagana,
Abdallah Mtoro ‘Dallas’ na huyu wa sasa ambaye bado hajamuanika jina,
wote eti wameshindwa kuzaa naye.
Chanzo: Risasi Jumamosi/Gpl
Chanzo: Risasi Jumamosi/Gpl