Msanii
wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka katika ukurasa wa Facebook wa
EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live na kusema kuwa yeye hajaachana
na mumeo wa ndoa na wala msanii Diamond Platnum hajavunja ndoa yao kama
ambavyo baadhi ya watu na vyombo vya habari walivyokuwa wakisema.
Uwoya
ameweka wazi suala hilo baada ya mashabiki wengi kutaka kujua kama
ameachana na mumeo ndikumana na ndipo hapo amekanusha kuwa hajawahi kuwa
na mahusiano na Diamond Platnum wala Msanii Msami Baby kama ambavyo
watu wamekuwa wakijua ni wapenzi bali amesema kuwa yeye na msanii Msami
ni marafiki wa karibu na sasa wanafanya filamu ya pamoja.