Chidi Benz alitabiri mbele ya Diamond Platnumz (wakati bado underground) kuwa angekuja kuwa msanii mkubwa.
Hata hivyo maneno muhimu ambayo rapper huyo alimwambia Diamond ni kuwa asije kunywa pombe wala kuvuta (unga/bangi) maishani mwake.
Chidi ambaye Jumanne hii ameachia single yake mpya 'Mpaka Kuche' aliyowashirikisha Diamond na AY, alikuwa akihojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM. Katika kuashiria kuwa hiyo ilikuwa ni interview iliyogusa sehemu ya katikati kabisa ya moyo wake, Chidi alijikuta akibubujikwa na machozi.
Chidi alikumbushia siku Diamond alipompigia simu kujitambulisha kwake kuwa ni msanii mchanga anayetaka kumshirikisha kwenye wimbo wake. Hata hivyo siku Diamond amefanikiwa kumpata Chidi hewani ilikuwa ni baada ya kujaribu kumtafuta kwa siku nyingi bila mafanikio na aliwahi kumweleza mama yake namna alivyo na hamu ya kumshirikisha rapper huyo aliyekuwa akimkubali.
Baada ya kumpigia simu, Chidi anadai alimuambia Diamond aende kwao maghorofani Ilala wakazungumze vizuri.
"Sasa nikamuona (Diamond) nikajua huyo dogo ndio yule niliwaambiaga watu kuwa ‘huyu dogo ana sura moja hivi imekaa.. sura yake lazima utaiongelea tu, lazima utasema kitu, namuona atakuja kuwa staa tu, simjui lakini the way alivyo, atakuja kuwa staa,” alikumbushia Chidi.
 
Top