0
Ijumaa (July 19) haikua siku nzuri kwa Naibu Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknolojia mh. January Makamba baada ya kupokea jumbe nyingi kutoka kwa baadhi ya wananchi muda mfupi baada ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika kuweka hadharini namba yake ya simu ya mkononi ili watu wampigie na kumhoji kuhusu tozo la kodi ya umiliki wa kadi za simu.
“Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni ……..) kwa kuwa yeye ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali.”aliandika Mnyika katika taarifa yake.

Mambo yalikuwa tofauti baada simu yake kugeuka kuwa ‘public suggestions box’ iliyobeba kila aina ya jumbe za ajabu na matusi huku wengine wakidiriki kumpigia kitu ambacho kiligeuka kero kwake.

Makamba alitumia ukurasa wake wa facebook kuelezea kile kilichomkuta huku akilaani kitendo alichokifanya Mh John Mnyika.

John Mnyika kaweka namba yangu ya simu ya mkononi ili watu wanipigie na kutukana. Nadhani ni siasa isiyo ya kistaarabu. Hadi sasa nimepata messages zaidi ya 600. Sio sahihi kabisa. Wabunge WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini. Harakati za mitandaoni haziondoi ukweli huo.” Ni sehemu ya alichokiandika Makamba.

Hata hivyo pamoja na hayo yote anaamini kuwa hayo yataisha hivyo asibadili namba yake ya simu. 

Nae dada yake January Makamba ‘Mwamvita Makamba’ alionesha kuumizwa na kile alichokifanya Mnyika na kumtumia ujumbe kupitia akaunti yake ya twitter akimtaka aombe radhi kwa kuwa yeye ni bora ya kile alichokifanya, na kwamba yeye ameziona jumbe zilizotumwa kwa kaka yake.
Uamuzi wa bunge kupitisha tozo la kodi ya kadi za simu kwa mwezi kwa wananchi umepingwa vikali na wananchi lakini pia asilimia kubwa ya wabunge wanaoulizwa kuhusu uamuzi huo nao wanaonekana kupinga hoja hiyo na wengine wakirusha lawama zao kwa ‘serikali’…Japo ukweli unabaki palepale kuwa wabunge (asilimia kubwa) ndio waliopitisha mswada huo bungeni.

 January Makamba anakiri kuwa wabunge walishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini.  
CHANZO : LEOTAINMENTTZ.COM

Wabunge WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini.” Aliandika Makamba katika sehemu ya ujumbe wake kupitia ukurasa wa facebook. 

BOFYA UWE MJANJA
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
BOFYA UWE MJANJA

Post a Comment Blogger

 
Top