0

Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu amejikuta kwenye wakati mgumu baada leo akaunti yake ya Facebook kuonesha imepost link yenye kichwa cha habari ‘Picha za uchi alizopiga Lady Jay D bofya hapa’. Kutokana na post hiyo, Adam amejikuta akitukanwa matusi mengi ya nguoni kitendo kilichomlazimu aombe radhi japo anadai hakuandika yeye.

adam

“Naomba kuchukua nafasi hii kuomba radhi kwa yeyote aliyekwazika kwa maneno machafu yaliyoandikwa kwa wall yangu, na pia naomba nieleweke kwamba sihusiki na chochote kupost au kuandika chochote kuhusu kikwete foundation na picha za jdee ukiwa naked, sina ugomvi na yeyote naheshimu hisia za kila mtu nikiamini kila mtu ana maamuzi yake.. Aliyeamua kutumia jina langu kufanya hayo najua sasa unajiskia vizuri baada ya matusi mengi niliyotukanwa.. Maisha hayaishii hapa siku zinaenda na ukwali utafahamika siku moja … Mchana mwema.”

“Mi namuachia Mungu … Ya duniani yatalipwa hapa hapa, anayetengeneza mazingira haya kunichafua ni baraka zinaongezeka .. I keep on moving sirusishwi nyuma na kauli zenu zilizojaa chuki, dharau maisha Yanaendelea.
Kiukweli napata lawama nyingi matusi mengi bila kujua kosa langu.. Account yangu ni hii sina nyingine na sijui nn kimeendelea huko, kiroho safi tu naomba mtu aniambie kuna nini wapi nijue ivi mtanilaumu bure tu.. No hard feelings.”

BOFYA UWE MJANJA
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
BOFYA UWE MJANJA

Post a Comment Blogger

 
Top